Namna gani tuna pashwa kusali
ENSEIGNANT : Paulin CHOKORO NDERHE
Passage biblique à
lire : Matthieu 5 : 15
Thème : Namna gani tuna pashwa kusali
Version swahili
1.
UKUMBUSHO WA SOMO LA SIKU YA
TATU (LILILO TOLEWA NA MWALIMU ZALUMIRE)
Je, ni wangapi leo
huomba ili wapate vitu? Wengi wetu, kwa masikitiko, ndio hivyo.
Yesu alivunja aina mbili za sala zisizo za kweli:
·
Sala
ya unafiki
(kuomba ili kuonekana),
·
Sala
ya kipagani
(kuomba ili kupata vitu kwa kulazimisha).
Katika hotuba (Ce
discours) hii, Yesu anaeleza sala ya
kweli:
Ni kilio cha mtoto kwa
Baba yake, (Un cri d’enfant au Père)
kinachomlenga Mungu,
(Centré sur Dieu)
huru kutokana na
ubinafsi, (Libéré de l’Ego)
chenye imani kwa
msaada wa Mungu, (Confiant dans la providence divine)
siyo mazoezi ya
kidini. (Pas un exercice religieux)
Kusifiwa, kuonyesha "ukaribu wao
wa kiroho" (Impressioner les autres) ; maneno ya kifahari, sala ndefu
katika mikutano, wakichanganya maneno ya ajabu na yasiyoeleweka, wakidai ni
"kunena kwa lugha" : Lakini Mungu anachukizwa
na haya. Yeye hamsikilizi
muigizaji, anamsikiliza mtoto
wake.
2. SOMO LA SIKU
Mfano Halisi wa Sala: Kumlenga Mungu, Siyo Mtu
Yesu anafundisha sala
tofauti kabisa na zile za kisasa:
Basi tusome
hapo : Matayo 6 :9-13.
1.
Baba
yetu uliye mbinguni
→ Siyo Mungu wa mbali, ni Baba
wetu, aliye juu ya yote.
Baba anakaa mbiguni,
(Zaburi 103 :19)
Amakuwa Baba yetu, nasi ni wana wake.
( Warumi 8 :15 Roho mtakatifu hushuudiwa moyoni mwetu ya kwamba
Mungu ni Baba Yetu)
1 Yohana
3 :1 ; Zaburi
103 :13 ;
BWana mwenyewe
ushuhudia : 2 wakorintho 6 :18.
2.
Jina
lako litukuzwe
→ Lengo la kwanza siyo
mafanikio yetu, ni utukufu wa Mungu.
Kusoma zaidi : Isaya
43 :7. Tuliumbwa kwa utukufu wa Bwana.
3.
Ufalme
wako uje
→ Lengo siyo
ufalme wetu, ni ufalme wa Bwana.
4.
Mapenzi
yako yatimizwe duniani kama mbinguni → Siyo matakwa (mapenzi) yangu, bali mapenzi ya
Baba.
Kila kitu kinaanza na Mungu. Siyo mimi.
Na baadaye ndipo tunaomba:
5.
Utupe leo riziki yetu ya
kila siku → Si utajiri, bali kinachotosha leo tu.
Matayo 6:31-33
Musiseme, tutakula
nini? Au tutakynya nini?.. bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake.
Na hayo yote muta zidishwa.
Zaburi 37 :25 « Sijawayi kuona mwenye haki ameachwa, wala
watoto wake wakiomba jiani »
6.
Tusamehe
makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea → Sala inadai unyenyekevu (l’humilité),
toba (La
repentance), na msamaha
(le pardon).
Matayo 18 :21-22 « Yesu
akamwabia, si kukuambia hata mara saba, bali hata mara sabini mara saba »
7.
Usitutie
majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu → Kilio cha kutegemea Mungu katika udhaifu wetu.
2 Petro 2:9
“Bwana anajua kuwaokoa wacha Mungu na majaribu”
Akuna kile
ambacho kina tu fikiya Bwana asiya ruhusu (Yobu 1:12)
Bwana
hatatujaribu kupitia imani yetu ( 1 wakorintho 10:13)
8.
Kwa kuwa Ufalme ni Wako, Na nguvu, na utukufu hata
milele amen
Ina mahanisha
nini hapo!
Ufalme : Ya kwamba yeye ndiye ana mamlaka duniani na mbiguni : Zaburi 103:19. (L’autorité
compétente)
Nguvu: Yakwamba tuna amini ya kuwa Mungu ndiye ana nguvu. Akuna kinacho
tendeka bila uwezo wake. (Mambo ya nyakati 29:11).
Utukufu : Ya kuwa anakuwa anatukuzwa, na pia ana itaji kusifiwa.
-
Sifa zote,
-
Heshima
-
Na ushindi ni kwake.
Hata milele: yani iyo siyo mambo ya Muda, Ufalme wake niwa milele (Danieli
7:14).
Sharti la Sala: Kusamehe kwa Moyo
"Kama hamtasamehe wanadamu, Baba yenu hatawasamehe ninyi pia makosa
yenu." (Mathayo 6:15)
Yesu anavunja
udanganyifu huo: hakuna ushirika wa kweli na Mungu kama tuna chuki na kinyongo
mioyoni mwetu.
Conclusion
Mkristo wa
kweli haombi ili kumtawala Mungu.
Anaomba kwa
sababu Mungu ni Baba yake — kwa upendo, kwa imani, na kwa unyenyekevu.
Lakini leo, sala
nyingi zimekuwa kama amri
(commandes) kwa Mungu:
·
"Natangaza,
naamuru, natabiri..."
Wazimu huu ni
nini? Wazimu kamili! (c’est de la folie, c’est contradictoire avec les
écritures).
Je, sisi ni nani wa kumwamuru Muumba wa ulimwengu?
"Mapenzi
yako yatimizwe."
Sala ya kweli
ni kujisalimisha, siyo kudai.
SWALI
KWA MUKUTANO
Utupe leo riziki zetu, je ni riziki za kiroho ama
za kimwili ? ama ni zote mbili ??
Utusamehe makosa yetu, je ombi hili linakuwa tena (une
déclaration de foi ??)
Katika mukutano ya wayahudi (katika utamaduni,
dans la culture), kumuita Mungu Baba ilikuwa jambo la atuwa kubwa (un acte
révolutionnaire), Je, ilikuwa tendo la imani ama la hatari ? na leo yii
lina tu fundisha nini ?
Je tunawezaje ku iishi mufano huu bila ku vunja
mantiki ya dunia ? (sans briser la logique du monde dominé par les injustices,
la vengeance, ??)
Commentaires
Enregistrer un commentaire
Laissez un commentaire